*AWF YAWAKUTANISHA WAFUGAJI NA MBUGA YA MKOMAZI ~ SAME.*
🔸Viongozi wa wafugaji kutoka Wilaya 5 za Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga wakutana kujadili juu ya maendeleo yao na jinsi wanavyoweza kushirikiana na Mkomazi ili kuboresha maisha yao.
🔸AWF waeleza dhamira yao ya kuona wafugaji wanajua faida ya Mkomazi na fursa kwao na kutaka kubadilisha maisha ya wafugaji kwa kufanya ufugaji wao kuwa na tija zaidi.
🔸Sheria za hifadhi zaelezwa zinazozuia mifugo kuingizwa hifadhini. Na jinsi wanavyohusiana na jamii inayowazunguka.
🔸Wafugaji waomba maeneo ya malisho kutengwa na kuwa na hati, waomba kujengewa mabwawa ya maji na huduma nyingine zitakazowezesha mifugo kupata huduma bila kuingia mbugani.
🔸DC Same Mh. Rosemary Senyamule aliyekuwa mgeni rasmi siku hiyo awaagiza kufanya vikao hivi walau mara moja kwa mwaka, pia kupeleka huduma zinazohusisha ufugaji.
Awataka wafugaji kushiriki ujenzi wa miundombinu yao, kuunda ushirika, kuzingatia sheria na kusomesha watoto ili baadaye wajue kufuga kisasa. Atoa ufafanuzi juu ya fursa iliyotolewa na Rais Mh. Dr. John Pombe Magufuli juu ya maeneo ya malisho katika hifadhi. Aeleza mpango mkakati wa utalii wa Wilaya na dhamira ya Wilaya kukuza utalii.
🔸Awashukuru AWF kwa kuwezwesha kikao kilichoonekana kuhitajika na kila upande. Awaomba kushiriki ujenzi wa miundombinu kwa wafugani.
🔸Kikao kilifanyika ukumbi wa Amani hostel ambapo Wilaya ya Same, Mwanga, Lushoto, Mkinga na Korogwe zilishiriki.
" *Same is not same"*
Picha ya Pamoja Baada ya Majadiliano ya Pamoja

*WAJASILIAMALI WADOGO SAME WAMPONGEZA RAIS*
Katika kuhamasisha vitambulisho vya wajasiliamali. Wajasiliamali wadogo wamemshukuru Rais Mh. Dr. John Pombe Magufuli kwani tangu wameanza kutumia vitambulisho hivyo. Wamefanya biashara kwa amani.
🔥DC Same akihamasisha uchukuaji wa vitambulisho hivyo kata ya Hedaru na Maore. Amewakumbusha dhamira njema ya Mh. Rais na faida watakayoipata kwa kuwa na vitambulisho hivyo.
🔥Awataka kamati ya mapato ya halmashauri kushauri ongezeko la ushuru kwani ina maanisha wale ambao bado hawajachukua vitambulisho ni wafanyabiashara wakubwa wenye mapato zaidi ya 4M kwa mwaka.
🔥Aagiza elimu ya vitambulisho iendelee kwani wengi bado wana maswali na wanahitaji ufafanuzi.
🔥" Hakikisheni mnachukua risiti kwa kila mnachonunua ili serikali ipate kodi halali na itoe huduma nzuri kwenu." asema DC Huyo.
Aahidi kuendelea kutoa elimu ya kodi na mapato mpaka wananchi wawe wazalendo na kuanza kulipa wenyewe. Pia kuchukua hatua kwa wakwepa kodi.
🔹Ni SACCOs ya Chama Cha Walimu Wilayani Same wakabidhi mashuka 100 Na mablanket 200 vyenye thamani ya Tshs. 2.89M, Katika hospitali ya Wilaya ya Same.
🔹Mkt. wa CWT SACCOS Same Ndugu Mchome aeleza mkakati wa chama wa kurudusha huduma kwa wateja wao na kuihudumia jamii, kila mwaka hutenga fedha kwa ajili ya kuhudumia jamii. Ambapo pia mwaka 2017 walitoa vifaa na kufikisha thamani zaidi ya 5M kwa vifaa vyote.
🔹Akipokea vifaa hivyo DC Same aliwapongeza kwani ni kati ya SACCOS zinazofanya vizuri Wilayani hapo kati ya SACCOS 31 zilizopo.
🔹Aliwataka watumishi kuendelea kujiunga nao kwa kuwa wanaikumbuka jamii inayowazunguka wanapopata faida.
Aliwataka hospitali kutunza vifaa hivyo ili vidumu.
" Sio leo tunayaona mashuka meupe kesho yamekuwa brawni"
🔹Awaomba wadau wengine kuiga mfano wao. Kwani hii inaonyesha kuunga mkono serikali ya Rais wetu mpendwa Mh. Dr. John Pombe Magufuli katika kuboresha huduma za afya.
🔹Naye Mganga mkuu wa Wilaya Dr. Andrew akiongea kwa niaba ya DED alisema kitaalam kitanda kimoja kinahitaji mashuka 6 kwa siku kwani yanabadilishwa kila yanapochafuka.
Ashukuru na kuahidi kuyatunza.
🔹Pia DC aeleza jinsi serikali ya awamu ya tano ilivyoongeza bajeti ya afya Wilayani na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo kwa kujiunga na bima ya afya.
🔹Akishukuru mmoja wa wakinamama aliwataka kina mama wengine kuendelea kutumia huduma za afya rasmi ili kupunguza madhara ya huduma zisizo rasmi.
Kweli Same kuna raha
" Same is not same"
💧Ni ziara kijiji cha Mhezi kuzindua ujenzi wa mradi wa Maji, unaofadhiliwa na Rotary Club ya Same, Ames noon - Ames - Iowa USA na Rotary international utakaogharimu zaidi ya Tshs 800 M hadi kukamilika kwake.
💧Waaanza kupanda miti eneo la chanzo cha maji ambapo miti rafiki ya maji ipatayo 75 imepandwa, kung'oa visiki eneo la kujenga tanki, Kuchimba barabara ya kupitisha malighafi na kubeba kokoto.
💧DC aondoka na mhalifu aliyekata miti kwenye chanzo na kutakiwa kulipa 4M kwa uharibifu huo.
💧Rais wa Rotary club tawi la Same Amon Noel Mchomvu ameahidi kuujenga mradi huo kwa miezi 15 na ameomba ushirikiano wa wananchi kwa kuchimba mitaro na ulinzi wa vifaa. Asema huu ni mradi wa 5 kwa miradi waliyoileta Same, aahidi kushirikiana na wananchi zaidi kuleta maendeleo.
💧DC Same Mh. Rosemary Senyamule awataka wananchi kutoa ushirikiano ili mradi huu uishe kwa wakati. Pia kutunza mazingira. Awataka Rotary kujenga kwa viwango na kuwa na uwazi ili mradi udumu muda mrefu. Mhandisi aagizwa kusimamia kwa karibu.
💧"Rotary mmekuwa marafiki wazuri wa Same. Tutaendelea kuwapa ushirikiano kwani mnafuata taratibu zote za serikali" asanteni sana. Alisema DC huyo.
💧Kazi hii ilileta furaha kwa viongozi wote waliohudhuria kwa kumaliza mwaka kwa kufanya kazi za maendeleo zenye tija kwa jamii. Na kuunga mkono kampeini ya Wilaya ijulikanayo kwa jina la
" *Kijiji changu, Furaha yangu"*
Ziara ilifanyika tar. 31/12/2018; DC aliongozana na wataalamu toka halmashauri.
" Same is not same"

Mkuu wa Wilaya ya Same. Akiwa na Rotarian wa Same Sambamba na wananchi katika zoezi la Uzinduzi wa Mradi wa Maji Kaika Kata ya Mhezi Kijiji cha Mhezi.

Mhe. Rosemary Mkuu wa wilaya ya Same Akipanda Mti wa Kumbukumbu katika zoezi la Uzinduzi wa Mradi wa Maji kata ya Mhezi Kijiji cha Mhezi

💠Kikao kilichoitishwa na Viongozi wa Wilaya ili kuweka mikakati ya kumaliza mwaka 2018 na kuanza mwaka 2019.
Kikao kilimuhusisha DC Same, DAS, DED, TAKUKURU, wakuu wa idara, A/tarafa, watendaji kata na vijiji. 7
💠Wakumbushwa kujituma, uaminifu na ukusanyaji mapato katika maeneo yao. Pia kuhakikisha wanatatua kero za wananchi kwa wakati. 
Wakumbushwa kukamilisha ujenzi wa madarasa kukidhi idadi ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza. Kufanya msaragambo kila j'tatu ili kuleta maendeleo kwa haraka.
💠DC Same Mh. Rosemary Senyamule aelezea mpango wa
" *Kijiji changu, Furaha yangu"*
Kama mpango anaofikiri ukitekelezwa kwa umakini na watendaji kuhamasisha maendeleo kwa bidii vijijini ni wazi maendeleo yatakuja kwa kasi.
" Kwa kuwa mwezi Disemba watu wengi wanarudi nyumbani, hebu tuwashirikishe maendeleo tuliyoyafanya na mipango tuliyonayo kwa ngazi za vijiji ili nao waone watashiriki namna gani" . Hayo yalisemwa na DC Same.
Ataka WEO kuleta taarifa ya viwanda kabla ya tar. 15/12/2018 kwa mpango wa kila kata kiwanda kimoja.
💠Pia DED Same alieleza jinsi walivyojipanga kukusanya mapato na matarajio aliyonayo ya kufikia lengo. Pia6 aliwasisitiza watendaji kuwa waadilifu kwenye mapato.
💠DAS alisisitiza swala la kumaliza mirungi kwa maeneo machache yaliyobaki ili kuwa na Same isiyo na mirungi.
Naye mwakilishi wa TAKUKURU ahimiza swala la kuweka fedha za serikali benki kabla ya kuzitumia na umuhimu wa kufuata sheria na taratibu.
💠 Umuhimu wa utekelezaji wa CCM wasisitizwa na kutoa taarifa ya utekelezaji wake. Ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe
Joseph Magufuli.
Tunategemea mwaka 2018 uwe mwaka wa mafanikio zaidi.
" *Same* *is* *not* *same* "
NGARITO TUKIFANYA SAME IMEFANYA
🔸Ni vijana 52 walioamua kukaa kambini kwa siku 5 mfululizo ili kuhakikisha wanakamilisha ufunguzi wa barabara itakayounganisha kitongoji cha Gavao ngarito, kata ya Gavao Saweni na kitongoji cha Gundusine kata ya Hedaru ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na usafirishaji wa mazao.
🔸DC Same aliungana na vijana hao kulima barabara pamoja na kukagua changamoto ya mawe makubwa yanayokwamisha ukamilishaji wa barabara hiyo.
🔸DC huyo aliongozana na meneja wa TARURA Wilaya ambaye pia aliahidi kuiingiza barabara hiyo kwenye mtandao kwani itaunganisha kata na kata.
🔸DC alichangisha hela za papo kwa papo kwa ajili ya kununua baruti za kupasulia mawe hayo.
🔸Cha kufurahisha ni masufuria makuubwa ya wali yaliyoongeza ari ya kufanya kazi.
🔸"Tunataka kuanzisha mpango wa kuimarisha vijiji kwa kujiletea maendeleo wenyewe, utakaojulikana kwa jina la 'KIJIJI CHANGU, FURAHA YANGU'. Kwani wananchi wengi wanaishi vijijini; na kuimarika kwa vijiji na huduma ndiyo furaha ya maisha yao". Alisema DC Rosemary Senyamule.
🔸Aliwapongeza wananchi na kuahidi kuhamasisha wengine waige mfano huo. Kwani kuimarika kwa kijiji kimoja kimoja ndiyo kuimarika kwa Wilaya. Alimpongeza diwani kwa mkakati huo.
🔸Pia aliwapoongeza kwa kutekeleza maagizo ya Rais wetu Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli ya kumtaka kila mtanznia afanye kazi.
" Same is not the same"