WILAYA YA SAME KUWA WILAYA YA KWANZA KUTENGENEZA MPANGO MKAKATI WA MAZINGIRA NA UTALII 2018-2023

Uzinduzi Ulifanyika katika kilele cha mlima shengena kwenye hifadhi ya msitu wa Chome umbali wa km 2462 toka usawa wa bahari. Washiriki 160 wapewa cheti cha kufika kileleni. 
🌲Mpango wa mazingira utaunganisha Mbuga ya Mkomazi, msitu wa Chome, kilele cha Shengena na utalii wa asili. Kutengeneza kifurushi (package) cha utalii na kuipa jina maalumu (brand).
🌲Utekelezaji wa mpango kuifanya Same kuwa kivutio cha pekee na kuongeza idadi ya watalii.
🌲Mpango wa mazingira kutumika kuunganisha wadau kuibadilisha Wilaya ya Same. 
🌲Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akimwakilisha Waziri. Pamoja na kupongeza juhudi za Wilaya ya Same. Aahidi kushirikiana na Wilaya kutekeleza mipango hiyo kwani kitu wanachofanya ni kati ya vipaumbele vya serikali kwa kuimarisha utalii katika maeneo mengi ili yaweze kujitegemea. ðŸŒ²Naye CEO wa TFS Prof. Silayo aeleza adhma ya kuimarisha utalii wa ikolojia katika msitu huo ili uweze kuongeza mapato kwa wananchi kushiriki na serikali.🌲Mkurugenzi wa TANAPA aahidi kushirikiana na TFS kutangaza utalii wa Mkomazi na Shengena ili kuvutia zaidi watalii.🌲Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango Dodoma Prof. Israel Katega aahidi kushiriki na kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kama walivyosaidia katika kuutengeneza. ðŸŒ²Mwakilishi wa UNDP aahidi kusaidia utekelezaji wa mpango.🌲Naye Mwakilishi wa RC Kilimanjaro Mh. Kippi Warioba asema jambo hili ni la kuigwa na Wilaya nyingine. Apongeza, aahidi kutangaza utalii wa shengena. 
🌲Shughuli hiyo pia ilihudhuriwa na DC Siha, Mkt. CCM W., DAS Hai, Wiz. TAMISEMI, Mazingira, Utalii, NEMC, wawakilishi wa Mkoa, Mkomazi, NGO, Benki, wanasame waishio nje ya Same, na viongozi ngazi zote za Wilaya ambao kwa umoja wao waliahidi kutekeleza mpango.
🌲" Shukrani yetu kwa waliotengeneza mipango hii na mliohudhuria leo ni kuhakikisha mipango hii haikai kabatini, tutaitekeleza na kuhakikisha inachangia kuleta maendeleo ya haraka kwa Wilaya ya Same. Asanteni mno" . Hayo yalisemwa na DC Same Mh Rosemary Senyamule 
Hakika
"Same is not the same"

Hapa Baadhi ya Washiriki wakiwa Katika Mazingira ya Kilele cha Mlima Shengena
Picha ya Pamoja Ya Viongozi na Wawakilishi