Kiutawala Wilaya imegawanyika katika Tarafa 6, Kata 34, Mamlaka ya Mji Mdogo 1, Vijiji 100, Vitongoji 496, na mitaa 16 inayounda Mamlaka ya Mji mdogo wa Same na ina Halmashauri moja ambayo ilianzishwa 01 Januari 1984. Aidha kuna majimbo mawili ya Uchaguzi ambayo ni Same Mashariki yenye (Tarafa 3, Kata 14, vijiji 49, na vitongoji 214) na Same Mashariki yenye (Tarafa 3, Kata 20, Vijiji 51, Vitongoji 282 na mitaa 16). Wilaya iko kwenye mwinuko wa futi 1100 hadi 2462 kutoka usawa wa baharí.