Wilaya ya Same ni moja kati ya Wilaya sita (7)
za Mkoa wa Kilimanjaro. Ilianzishwa Mwaka 1962. Wilaya ina ukubwa wa kilomita za mraba 5,186 sawa na asilimia 39 ya eneo la
Mkoa wa Kilimanjaro na hivyo kuifanya kuwa Wilaya kubwa kuliko zote zinazounda Mkoa huu.
Wilaya ya Same inakadiriwa kuwa na Wakazi
wapatao 291,145 na idadi ya kaya zipatazo 64,699 kwa matoleo ya 15 Desemba 2015
kutokana na ongezeko (projections) la 1.8% kwa mujibu wa sensa ya watu na
makazi ya mwaka 2012. Kati ya hawa wanawake ni 149,229 (51.3%) na wanaume ni
141,916 (48.7%). Msongamano wa watu (Population Density) ni watu 56 kwa
kilomita ya mraba.
Kutokana na utafiti wa kiuchumi wa mwaka
2005, Pato la Mkazi (Income per capital) lilionekana kuwa ni shilingi 436,900
kwa mwaka, kwa mtazamo wa kipato (income approach) cha mkazi, kiasi ambacho kwa sasa kinakadiriwa kufikia
wastani wa shilingi 720,000 kwa mwaka.
MGAWANYO WA
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Tumeigawa
wilaya yetu kutokana na jiografia yake katika shughuli za kiuchumi ili
itusaidie kuwa na “focus”
Eneo
moja linaweza likajirudia mara mbili au zaidi kulingana na hali yake na
uhitaji.
1. Kilimo:
Tangawizi/Kahawa(Milimani)
- Mpinji –Tae
- Mamba Myamba
- Bwambo – Vudee
- Mtii – Suji
- Lugulu – Mshewa
- Chome – Kirangare
- Bombo – vutata
- Msindo – miheri
Korosho/Mkonge(Tambarare)
- Njoro
- Makanya
- Hedaru
- Mwembe
- Bangalele
- Kisiwani
- Mabilioni
Mboga mboga (Hortculture)
- Ruvu
- Mabilioni
- Chome
- Kisiwani
- Maore
- Kalemawe
Umwagiliaji Mpunga
- Ndungu
- Kalemawe
- Bendera
- Maore
Ufugaji wa wanyama
- Njoro
- Ruvu
- Makanya
- Hedaru
- Mabilioni
- Kalemawe
Samaki
- Kalemawe
- Ruvu
- Maore
- Kisiwani
Utalii/Taasisi
- Same
- Mshewa
- Stesheni
- Kisima
- Vilimani
- Kisiwani
- Njoro
- Bombo
- Chome
- Tae
- Mtii
- Vuje
Madini
- Bendera
- Makanya
- Hedaru
- Mabilioni
- Kalemawe
- Mwembe/Bangalala
Viwanda/Taasisi/Uwekezaji
- Mwembe
- Makanya
- Bangalala
- Hedaru
- Njoro
- Mabilioni
- Ruvu