Ni kikao cha wafanyabiashara Same na DC Same pamoja na watendaji wengine wa taasisi za serikali.
- Waeleza kero na vikwazo katika biashara.
- Swala la lugha za watendaji lalalamikiwa zaidi.
- Makadirio ya kodi nalo lasemwa.
- Wataalamu toka TRA, TBS, TIC, TCCIA, Halmashauri na mamlaka ya mji mdogo watoa maelezo na majibu ya kero.
- DC aeleza matarajio ya serikali kwa wafanyabiashara - kila mtu alipe kodi yake.
- Awataka kujituma na kuchangamkia fursa ya viwanda hata vidogo kwani dhamira ni kuona waTanzania wengi zaidi wanamiliki viwanda.
- Kwa kuwa Rais wetu Mh Dr. John Pombe Joseph Magufuli amedhamiria kutumia vizuri fedha ya serikali kuwaletea wananchi maendeleo; awataka waunge mkono juhudi zake kwa kutoa risiti ili walipe kodi halali.
- Aeleza fursa za uwekezaji zilizopo na mipango ya Wilaya kukuza biashara na uchumi.
- Awashauri kujiunga na TCCIA ili wapate sauti ya pamoja. na awataka kuchagua wajumbe wa baraza la biashara.
- Aahidi kufanya kikao cha baraza mwezi Mei, 2018.
Picha ya Pamoja Mara Baada ya Kikao |
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkt. TCCIA - W., Mkt. wa halmashauri na kaimu DED, Mkiti wa mamlaka ya mji mdogo na TEO. Pia wakuu wa idara za Halmashauri. Kilifanyika Tar. 27/03/2017 Katika ukumbi wa Kimweri.
Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Mwigulu Lameck Nchemba Awa Waziri wa kwanza kufika Kijiji cha Makasa, Kata ya Kirangare, Wilaya ya Same.
- Apanda milima ambayo wengi wanaigopa.
- Ahimiza Umuhimu wa amani na kila mtu kuhakikisha inalindwa.
- Atangaza hatari kwa wastawishaji wa mirungi, kwani sheria mpya inaruhusu kutaifisha mashamba.
- Ashiriki Harambee ya ujenzi wa kanisa.
- Wananchi waipongeza serikali ya awamu ya Tano, kwani hawajawahi kutembelewa na Waziri.
- Wananchi waomba asaidie kuiomba serikali watengenezewe barabara.
- Naye Askofu Mjema wa KKKT Dayosisi ya Pare Apongeza kazi nzuri inayofanywa na serikali
Mh. Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, akiwa katika Picha ya Pamoja Mara Baada ya Kumalizika kwa Ibada. |
TAHOSA YAPANIA KUPANDISHA UFAULU SAME.
Kikao cha Wakuu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Same chafanyika Tar. 21/03/2018.
Kikao cha Wakuu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Same chafanyika Tar. 21/03/2018.
- 🔰 Wakusudia kutoka nafasi 21 hadi ya kumi bora kitaifa..
- 🔰Wajipongeza kuongeza ufaulu toka nafasi ya 68 hadi 21.
- 🔰Waeleza changamoto ya utoro wa wanafunzi kama kikwazo cha ufaulu.
- 🔰Wamuomba DC kuwa mlezi wao.
DC Same aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kikao hizo afanya yafuatayo.
- Atoa zawadi kwa shule 3 za kwanza kwa ujumla na 3 za serikali
- Awapongeza waliofanya vizuri kwa kuungana na kauli ya Same ya kutaka mabadiliko.
- DC aeleza baadhi ya sababu zinazopelekea shule za binafsi kufanya vizuri kuliko za serikali
- Asema pia uzembe wa baadhi ya walimu ni changamoto. Atoa Mf. wa matokei ya 2016 ambapo baada ya hesabu somo lililofuata kwa matokeo mabaya ni history ambayo ina walimu hadi wa ziada; haina practical lakini bado wameshindwa kuwaelewesha watoto.
- Atoa wito kwa walimu wazembe kukaza buti kudhihirisha uwezo wao kwa vitendo. Maana siku zao zinahesabika.
- Awakumbusha kumtendea haki Rais wetu Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali na watanzania kwani ameboresha Elimu pamoja na kuwapa posho ya madaraka.
- Awataka WEO/ VEO kuwaelimisha wazazi juu ya chakula cha mchana ili wakae muda mwingi mchana wakiwa na uangalizi wa shule.
- Agawa kitabu cha maadili ya watoto wa kike kwa kila shule, na awaomba walimu kuendelea kuwaelimisha ili kuondokana na mimba.
- Apongeza kwa takwimu zinazoashiria kupungua kwa mimba kulinganisha na 2017.
- Awataka shule zilizofanya vibaya kujithathmini ili kuongeza ufaulu.
- Awakumbusha shule binafsi kubadilishana uzoefu na wenzao ili kufanya vizuri kama taifa.
" Huko nyuma matokeo yalipokuwa mabaya, kila mtu alimtaja mwenzake kuwa ndiye aliyefanya uzembe( walimu walisema ni serikali na wazazi; wazazi walisema ni walimu na serikali; na serikali tumesema ni wazazi na walimu wazembe;
Lakini sasa tumefanya vizuri kila ninayekutana naye anaeleza jinsi alivyochangia /Alivyohusika na ufaulu huo, na kama ni hivyo basi kila mtu akubali pia alihusika kwa kufanya vibaya". Asema DC Same Mh. Rosemary Senyamule.
Lakini sasa tumefanya vizuri kila ninayekutana naye anaeleza jinsi alivyochangia /Alivyohusika na ufaulu huo, na kama ni hivyo basi kila mtu akubali pia alihusika kwa kufanya vibaya". Asema DC Same Mh. Rosemary Senyamule.
- Awataka wadau wote kutimiza wajibu wao, ili tujivunie matokeo mazuri kwa pamoja.
- Tanzania ya viwanda inahitaji wataalamu.
" Same is not same"
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Same akiwa na Wajumbe wa YAHOSA mara baada ya Kikao. |
NGO ya VOEWOF yadhamiria kuimarisha matumizi ya nishati mbadala Wilayani Same..
Katika kikao kilichofanyika Tar 20/03/2018. Wadau wa mazingira walieleza sababu zinazopelekea watu kutochangamkia nishati mbadala pamoja na juhudi za serikali na wadau kuhimiza matumizi yake.
Baadhi ya sababu zinazotajwa ni:-
- Kutopatikana nishati hiyo vijiji Mf. gas
- Gharama kubwa ya nishati mbadala, pia kodi katika bidhaa hizo.
- Mazoea na utamaduni
- 💡Wadau wakubaliana kuongeza matumizi, kubuni na kuanzisha nishati mbadala yenye gharama nafuu,
- 💡kuendelea kuelimisha juu ya athari ya mazingira na uwepo wa nishati mbadala.
- 💡Kuhimiza matumizi ya "interlocking block" badala ya tofari za kuchoma.
- 💡Kusimamia sheria.
- 💡Shirika la VOEWOF linalofanya kazi chini ya CARE International linafanya kazi na vikundi vya wanawake.
- 💡limewezesha majiko ya gas zaidi ya 300 kutumika vijijini.
- 💡Limepania kuanzisha viwanda vya kutengeneza nishati mbadala kwa kutumia taka.
- 💡Wilaya yaahidi kutoa eneo, kutoa mikopo kwa vikundi hivyo na kutumia miti inayooteshwa na vikundi hivyo.
Kikao hicho pia kimewashirikisha DC wa Same, wataalamu toka ofisi ya RC Kilimanjaro na halmashauri ya Same, TBS, wanazuoni toka SUA, TRA, wauzaji wa nishati mbadala, wanavikundi hao na vyombo vya habari.
DC Same alipongeza na kuwashukuru VOEWOF Na wadau wengine jinsi wanavyoshiriki kuibadilisha Same, kila mmoja kwenye nyanja yake. Alikiri kuwa kwa kasi hii; Wilaya ya Same itafikia malengo yake ya kubadili mazingira ya Same.
" Same is not same"