NGARITO TUKIFANYA SAME IMEFANYA
🔸Ni vijana 52 walioamua kukaa kambini kwa siku 5 mfululizo ili kuhakikisha wanakamilisha ufunguzi wa barabara itakayounganisha kitongoji cha Gavao ngarito, kata ya Gavao Saweni na kitongoji cha Gundusine kata ya Hedaru ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na usafirishaji wa mazao.
🔸DC Same aliungana na vijana hao kulima barabara pamoja na kukagua changamoto ya mawe makubwa yanayokwamisha ukamilishaji wa barabara hiyo.
🔸DC huyo aliongozana na meneja wa TARURA Wilaya ambaye pia aliahidi kuiingiza barabara hiyo kwenye mtandao kwani itaunganisha kata na kata.
🔸DC alichangisha hela za papo kwa papo kwa ajili ya kununua baruti za kupasulia mawe hayo.
🔸Cha kufurahisha ni masufuria makuubwa ya wali yaliyoongeza ari ya kufanya kazi.
🔸"Tunataka kuanzisha mpango wa kuimarisha vijiji kwa kujiletea maendeleo wenyewe, utakaojulikana kwa jina la 'KIJIJI CHANGU, FURAHA YANGU'. Kwani wananchi wengi wanaishi vijijini; na kuimarika kwa vijiji na huduma ndiyo furaha ya maisha yao". Alisema DC Rosemary Senyamule.
🔸Aliwapongeza wananchi na kuahidi kuhamasisha wengine waige mfano huo. Kwani kuimarika kwa kijiji kimoja kimoja ndiyo kuimarika kwa Wilaya. Alimpongeza diwani kwa mkakati huo.
🔸Pia aliwapoongeza kwa kutekeleza maagizo ya Rais wetu Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli ya kumtaka kila mtanznia afanye kazi.
" Same is not the same"