Uzinduzi Ulifanyika katika kilele cha mlima shengena kwenye hifadhi ya msitu wa Chome umbali wa km 2462 toka usawa wa bahari. Washiriki 160 wapewa cheti cha kufika kileleni. 
🌲Mpango wa mazingira utaunganisha Mbuga ya Mkomazi, msitu wa Chome, kilele cha Shengena na utalii wa asili. Kutengeneza kifurushi (package) cha utalii na kuipa jina maalumu (brand).
🌲Utekelezaji wa mpango kuifanya Same kuwa kivutio cha pekee na kuongeza idadi ya watalii.
🌲Mpango wa mazingira kutumika kuunganisha wadau kuibadilisha Wilaya ya Same. 
🌲Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akimwakilisha Waziri. Pamoja na kupongeza juhudi za Wilaya ya Same. Aahidi kushirikiana na Wilaya kutekeleza mipango hiyo kwani kitu wanachofanya ni kati ya vipaumbele vya serikali kwa kuimarisha utalii katika maeneo mengi ili yaweze kujitegemea. ðŸŒ²Naye CEO wa TFS Prof. Silayo aeleza adhma ya kuimarisha utalii wa ikolojia katika msitu huo ili uweze kuongeza mapato kwa wananchi kushiriki na serikali.🌲Mkurugenzi wa TANAPA aahidi kushirikiana na TFS kutangaza utalii wa Mkomazi na Shengena ili kuvutia zaidi watalii.🌲Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango Dodoma Prof. Israel Katega aahidi kushiriki na kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kama walivyosaidia katika kuutengeneza. ðŸŒ²Mwakilishi wa UNDP aahidi kusaidia utekelezaji wa mpango.🌲Naye Mwakilishi wa RC Kilimanjaro Mh. Kippi Warioba asema jambo hili ni la kuigwa na Wilaya nyingine. Apongeza, aahidi kutangaza utalii wa shengena. 
🌲Shughuli hiyo pia ilihudhuriwa na DC Siha, Mkt. CCM W., DAS Hai, Wiz. TAMISEMI, Mazingira, Utalii, NEMC, wawakilishi wa Mkoa, Mkomazi, NGO, Benki, wanasame waishio nje ya Same, na viongozi ngazi zote za Wilaya ambao kwa umoja wao waliahidi kutekeleza mpango.
🌲" Shukrani yetu kwa waliotengeneza mipango hii na mliohudhuria leo ni kuhakikisha mipango hii haikai kabatini, tutaitekeleza na kuhakikisha inachangia kuleta maendeleo ya haraka kwa Wilaya ya Same. Asanteni mno" . Hayo yalisemwa na DC Same Mh Rosemary Senyamule 
Hakika
"Same is not the same"

Hapa Baadhi ya Washiriki wakiwa Katika Mazingira ya Kilele cha Mlima Shengena
Picha ya Pamoja Ya Viongozi na Wawakilishi 



Kamati ya Lishe yazinduliwa Wilayani Same. Yahimizwa kuhakikisha Inapunguza kiasi cha udumavu Kutoka 29% ya sasa, ambayo Ndiyo ya Mkoa mzima wa Kilimanjaro.
Tanzania ya viwanda Na ya uchumi wa kati inataka watu wenye Lishe bora watakao kuwa Na akili nyingi, wabunifu Na wenye vipaji vya kufanya mambo makubwa. Yote hayo yanachangiwa Na Lishe bora. 
Alisema DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo Uliofanyika Tar. 07/09/2018.

Aliyesima ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Same na Upande wa  Kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same Dr. Andrew na Upande wa kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu AnnaCaire Shija.

  • Ni katika Ziara yake ya kutembelea nchi za Afrika iliyoanzia nchini Namibia, Tanzania na baadaye Kenya na kwingine. 
  • Akaa Tanzania siku nyingi zaidi. Na katika siku hizo 3; siku 2 apata mapumziko binafsi Wilayani Same, eneo la Mkomazi. 
  •  Afurahia mazingira ya asili yaliyoko Mkomazi aahidi kurudi tena. 
  • Aonyesha dhamira ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili aahidi kushiriki ukuzaji wa utalii kwa mipango ya Wilaya na TANAPA. Akumbusha utalii kuhusisha wananchi wanaozunguka hifadhi.
  • Mkomazi yatabiriwa kuwa kati ya hifadhi zenye mvuto mkubwa Africa kwa kuzingatia utekelezaji wa mipango mikubwa ya kuiboresha inayoendelea.
  • DC Same Mh. Rosemary Senyamule aeleza ukamilishaji wa mpango mkakati ya kukuza utalii Wilayani utakao unganisha utalii wa Mkomazi National Park, Mlima Shengena, msitu wa Chome pamoja na utalii wa asili/ utamaduni. (Yajayo yanafurahisha). Pia alimueleza fursa za uwekezaji zilizopo pamoja na kumkaribisha kuwekeza. 
  • aye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Dr. Allan Kijazi amueleza juu ya hifadhi za TANAPA na uhitaji ya kuongeza nguvu ya kupambana na ujangili. Amkaribisha kutembelea mbuga nyingine. Ampa zawadi za kumbukumbu.
    Mapokezi hayo Wilayani Same pia yalihudhuriwa na muhifadhi Mkuu wa Mkomazi ndugu Abel Msuya, Mr. Tonny ambaye ni mhidhadhi upande wa faru pamoja na Dr. Benard Mchomvu ambaye ni Mkt. Wa bodi ya uhifadhi wa faru. 
  • DC Same ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau wengine kutembelea Mkomazi.