- Ni katika Ziara yake ya kutembelea nchi za Afrika iliyoanzia nchini Namibia, Tanzania na baadaye Kenya na kwingine.
- Akaa Tanzania siku nyingi zaidi. Na katika siku hizo 3; siku 2 apata mapumziko binafsi Wilayani Same, eneo la Mkomazi.
- Afurahia mazingira ya asili yaliyoko Mkomazi aahidi kurudi tena.
- Aonyesha dhamira ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili aahidi kushiriki ukuzaji wa utalii kwa mipango ya Wilaya na TANAPA. Akumbusha utalii kuhusisha wananchi wanaozunguka hifadhi.
- Mkomazi yatabiriwa kuwa kati ya hifadhi zenye mvuto mkubwa Africa kwa kuzingatia utekelezaji wa mipango mikubwa ya kuiboresha inayoendelea.
- DC Same Mh. Rosemary Senyamule aeleza ukamilishaji wa mpango mkakati ya kukuza utalii Wilayani utakao unganisha utalii wa Mkomazi National Park, Mlima Shengena, msitu wa Chome pamoja na utalii wa asili/ utamaduni. (Yajayo yanafurahisha). Pia alimueleza fursa za uwekezaji zilizopo pamoja na kumkaribisha kuwekeza.
- aye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Dr. Allan Kijazi amueleza juu ya hifadhi za TANAPA na uhitaji ya kuongeza nguvu ya kupambana na ujangili. Amkaribisha kutembelea mbuga nyingine. Ampa zawadi za kumbukumbu.
Mapokezi hayo Wilayani Same pia yalihudhuriwa na muhifadhi Mkuu wa Mkomazi ndugu Abel Msuya, Mr. Tonny ambaye ni mhidhadhi upande wa faru pamoja na Dr. Benard Mchomvu ambaye ni Mkt. Wa bodi ya uhifadhi wa faru. - DC Same ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau wengine kutembelea Mkomazi.
PRINCE WILLIAM AICHAGUA SAME KWA MAPUMZIKO
posted by Wilaya ya Same
on 3:26 AM