💠Kikao kilichoitishwa na Viongozi wa Wilaya ili kuweka mikakati ya kumaliza mwaka 2018 na kuanza mwaka 2019.
Kikao kilimuhusisha DC Same, DAS, DED, TAKUKURU, wakuu wa idara, A/tarafa, watendaji kata na vijiji. 7
💠Wakumbushwa kujituma, uaminifu na ukusanyaji mapato katika maeneo yao. Pia kuhakikisha wanatatua kero za wananchi kwa wakati. 
Wakumbushwa kukamilisha ujenzi wa madarasa kukidhi idadi ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza. Kufanya msaragambo kila j'tatu ili kuleta maendeleo kwa haraka.
💠DC Same Mh. Rosemary Senyamule aelezea mpango wa
" *Kijiji changu, Furaha yangu"*
Kama mpango anaofikiri ukitekelezwa kwa umakini na watendaji kuhamasisha maendeleo kwa bidii vijijini ni wazi maendeleo yatakuja kwa kasi.
" Kwa kuwa mwezi Disemba watu wengi wanarudi nyumbani, hebu tuwashirikishe maendeleo tuliyoyafanya na mipango tuliyonayo kwa ngazi za vijiji ili nao waone watashiriki namna gani" . Hayo yalisemwa na DC Same.
Ataka WEO kuleta taarifa ya viwanda kabla ya tar. 15/12/2018 kwa mpango wa kila kata kiwanda kimoja.
💠Pia DED Same alieleza jinsi walivyojipanga kukusanya mapato na matarajio aliyonayo ya kufikia lengo. Pia6 aliwasisitiza watendaji kuwa waadilifu kwenye mapato.
💠DAS alisisitiza swala la kumaliza mirungi kwa maeneo machache yaliyobaki ili kuwa na Same isiyo na mirungi.
Naye mwakilishi wa TAKUKURU ahimiza swala la kuweka fedha za serikali benki kabla ya kuzitumia na umuhimu wa kufuata sheria na taratibu.
💠 Umuhimu wa utekelezaji wa CCM wasisitizwa na kutoa taarifa ya utekelezaji wake. Ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. John Pombe
Joseph Magufuli.
Tunategemea mwaka 2018 uwe mwaka wa mafanikio zaidi.
" *Same* *is* *not* *same* "
NGARITO TUKIFANYA SAME IMEFANYA
🔸Ni vijana 52 walioamua kukaa kambini kwa siku 5 mfululizo ili kuhakikisha wanakamilisha ufunguzi wa barabara itakayounganisha kitongoji cha Gavao ngarito, kata ya Gavao Saweni na kitongoji cha Gundusine kata ya Hedaru ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na usafirishaji wa mazao.
🔸DC Same aliungana na vijana hao kulima barabara pamoja na kukagua changamoto ya mawe makubwa yanayokwamisha ukamilishaji wa barabara hiyo.
🔸DC huyo aliongozana na meneja wa TARURA Wilaya ambaye pia aliahidi kuiingiza barabara hiyo kwenye mtandao kwani itaunganisha kata na kata.
🔸DC alichangisha hela za papo kwa papo kwa ajili ya kununua baruti za kupasulia mawe hayo.
🔸Cha kufurahisha ni masufuria makuubwa ya wali yaliyoongeza ari ya kufanya kazi.
🔸"Tunataka kuanzisha mpango wa kuimarisha vijiji kwa kujiletea maendeleo wenyewe, utakaojulikana kwa jina la 'KIJIJI CHANGU, FURAHA YANGU'. Kwani wananchi wengi wanaishi vijijini; na kuimarika kwa vijiji na huduma ndiyo furaha ya maisha yao". Alisema DC Rosemary Senyamule.
🔸Aliwapongeza wananchi na kuahidi kuhamasisha wengine waige mfano huo. Kwani kuimarika kwa kijiji kimoja kimoja ndiyo kuimarika kwa Wilaya. Alimpongeza diwani kwa mkakati huo.
🔸Pia aliwapoongeza kwa kutekeleza maagizo ya Rais wetu Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli ya kumtaka kila mtanznia afanye kazi.
" Same is not the same"








Uzinduzi Ulifanyika katika kilele cha mlima shengena kwenye hifadhi ya msitu wa Chome umbali wa km 2462 toka usawa wa bahari. Washiriki 160 wapewa cheti cha kufika kileleni. 
🌲Mpango wa mazingira utaunganisha Mbuga ya Mkomazi, msitu wa Chome, kilele cha Shengena na utalii wa asili. Kutengeneza kifurushi (package) cha utalii na kuipa jina maalumu (brand).
🌲Utekelezaji wa mpango kuifanya Same kuwa kivutio cha pekee na kuongeza idadi ya watalii.
🌲Mpango wa mazingira kutumika kuunganisha wadau kuibadilisha Wilaya ya Same. 
🌲Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo akimwakilisha Waziri. Pamoja na kupongeza juhudi za Wilaya ya Same. Aahidi kushirikiana na Wilaya kutekeleza mipango hiyo kwani kitu wanachofanya ni kati ya vipaumbele vya serikali kwa kuimarisha utalii katika maeneo mengi ili yaweze kujitegemea. 🌲Naye CEO wa TFS Prof. Silayo aeleza adhma ya kuimarisha utalii wa ikolojia katika msitu huo ili uweze kuongeza mapato kwa wananchi kushiriki na serikali.🌲Mkurugenzi wa TANAPA aahidi kushirikiana na TFS kutangaza utalii wa Mkomazi na Shengena ili kuvutia zaidi watalii.🌲Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango Dodoma Prof. Israel Katega aahidi kushiriki na kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kama walivyosaidia katika kuutengeneza. 🌲Mwakilishi wa UNDP aahidi kusaidia utekelezaji wa mpango.🌲Naye Mwakilishi wa RC Kilimanjaro Mh. Kippi Warioba asema jambo hili ni la kuigwa na Wilaya nyingine. Apongeza, aahidi kutangaza utalii wa shengena. 
🌲Shughuli hiyo pia ilihudhuriwa na DC Siha, Mkt. CCM W., DAS Hai, Wiz. TAMISEMI, Mazingira, Utalii, NEMC, wawakilishi wa Mkoa, Mkomazi, NGO, Benki, wanasame waishio nje ya Same, na viongozi ngazi zote za Wilaya ambao kwa umoja wao waliahidi kutekeleza mpango.
🌲" Shukrani yetu kwa waliotengeneza mipango hii na mliohudhuria leo ni kuhakikisha mipango hii haikai kabatini, tutaitekeleza na kuhakikisha inachangia kuleta maendeleo ya haraka kwa Wilaya ya Same. Asanteni mno" . Hayo yalisemwa na DC Same Mh Rosemary Senyamule 
Hakika
"Same is not the same"

Hapa Baadhi ya Washiriki wakiwa Katika Mazingira ya Kilele cha Mlima Shengena
Picha ya Pamoja Ya Viongozi na Wawakilishi 



Kamati ya Lishe yazinduliwa Wilayani Same. Yahimizwa kuhakikisha Inapunguza kiasi cha udumavu Kutoka 29% ya sasa, ambayo Ndiyo ya Mkoa mzima wa Kilimanjaro.
Tanzania ya viwanda Na ya uchumi wa kati inataka watu wenye Lishe bora watakao kuwa Na akili nyingi, wabunifu Na wenye vipaji vya kufanya mambo makubwa. Yote hayo yanachangiwa Na Lishe bora. 
Alisema DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo Uliofanyika Tar. 07/09/2018.

Aliyesima ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Same na Upande wa  Kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Same Dr. Andrew na Upande wa kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu AnnaCaire Shija.

  • Ni katika Ziara yake ya kutembelea nchi za Afrika iliyoanzia nchini Namibia, Tanzania na baadaye Kenya na kwingine. 
  • Akaa Tanzania siku nyingi zaidi. Na katika siku hizo 3; siku 2 apata mapumziko binafsi Wilayani Same, eneo la Mkomazi. 
  •  Afurahia mazingira ya asili yaliyoko Mkomazi aahidi kurudi tena. 
  • Aonyesha dhamira ya kusaidia mapambano dhidi ya ujangili aahidi kushiriki ukuzaji wa utalii kwa mipango ya Wilaya na TANAPA. Akumbusha utalii kuhusisha wananchi wanaozunguka hifadhi.
  • Mkomazi yatabiriwa kuwa kati ya hifadhi zenye mvuto mkubwa Africa kwa kuzingatia utekelezaji wa mipango mikubwa ya kuiboresha inayoendelea.
  • DC Same Mh. Rosemary Senyamule aeleza ukamilishaji wa mpango mkakati ya kukuza utalii Wilayani utakao unganisha utalii wa Mkomazi National Park, Mlima Shengena, msitu wa Chome pamoja na utalii wa asili/ utamaduni. (Yajayo yanafurahisha). Pia alimueleza fursa za uwekezaji zilizopo pamoja na kumkaribisha kuwekeza. 
  • aye Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Dr. Allan Kijazi amueleza juu ya hifadhi za TANAPA na uhitaji ya kuongeza nguvu ya kupambana na ujangili. Amkaribisha kutembelea mbuga nyingine. Ampa zawadi za kumbukumbu.
    Mapokezi hayo Wilayani Same pia yalihudhuriwa na muhifadhi Mkuu wa Mkomazi ndugu Abel Msuya, Mr. Tonny ambaye ni mhidhadhi upande wa faru pamoja na Dr. Benard Mchomvu ambaye ni Mkt. Wa bodi ya uhifadhi wa faru. 
  • DC Same ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau wengine kutembelea Mkomazi.
SAME DISTRICT COMMISSIONER PLANS “TO BRING THE WORLD TO SAME”
Letter from Moshi, Mkomazi, Ngorongoro, Serengeti and Zanzibar,
Invoking her most popular slogan of “Same is not same”, H.E. Rosemary Seyamule cut teeth with Tanzania’s with Vocational Education and Training Authority (VETA) and the government system to groom leadership from the ruling party’s hierarchy.
As a faithful leader, H.E Sayamule’s aspiration is to implement CCM party’s election manifesto to stir up developments in Same district that would change the “Lives” of her subjects.
Hosting a group of investors from both Tanzania and the USA, at her office yesterday, the Same District Commissioner articulated government’s policies and plans for investments to spawn efficient skilled labor force for both industries and services sector.
Same as the district would be the “HUB” of trained skilled labor force that would provide expertise to other regions of Tanzania and outside its border.
The group of investors from the USA and Tanzania paid a courtesy visit to the district commissioner in line-with her government’s initiatives to attract direct investments to Same.
She briefed the group about the plan to develop the Master-Plan for investors that would make Same the Switzerland of East Africa due to its potential to provide Paragliding/Parasailing based on Sports Tourism.
Same has the same scenery like Switzerland where the Alps mountain attract score of thousands tourists throughout the year. Same has the highest point where you can observe Mount Kilimanjaro clearly.
Her governments plan is to develop infrastructure that would make it easy for tourists to comfortable enjoy the scenery of Same city.
Cultural Tourism, one of the governments “Cash Cows” would be a motivating force in Same’s long term plans.
The USA group hinted that it would direct investment portfolios that would focus on the cutting-ege of education as a focal point.
Basing on the vocational and higher education, Same would transform into a major skilled labor force for Tanzania industrialization that is targeting the country to become a middle class economy by 2053.
The inherent values of Same district is its wealth of several natural resonances from Mkomazi National Park to gemstones, arable land for major commercial farming and attractive educational base.
It is its strategic position with a seat on the Cape Town to Cairo highway that makes this developing district of Tanzania a major investment destination in East Africa.
There would be more consultation with the USA group and also plenty of work to be by the government to realize Same’s aspiration as the Investment HUB in East Africa that would enable it to export skilled-labor and accommodating thousands of educational enthusiasts.
Indeed Same is not same and as the slogan gathers momentum, there is nothing to stop this important district of Tanzania to become the Switzerland of east Africa.
They call it Africa, We call it Home!


Ni kikao cha wafanyabiashara Same na DC Same pamoja na watendaji wengine wa taasisi za serikali. 
  •  Waeleza kero na vikwazo katika biashara.
  • Swala la lugha za watendaji lalalamikiwa zaidi.
  • Makadirio ya kodi nalo lasemwa. 
  •   Wataalamu toka TRA, TBS, TIC, TCCIA, Halmashauri na mamlaka ya mji mdogo watoa maelezo na majibu ya kero. 
  • DC aeleza matarajio ya serikali kwa wafanyabiashara - kila mtu alipe kodi yake. 
" Ni lazima tufuatilie kodi kwa kuwa watu hawana utamaduni wa kulipa; kama zaka tu watu wanamwibia MUNGU; Iwaje kodi ya serikali!!!"Alisema DC Rosemary Senyamule.
  • Awataka kujituma na kuchangamkia fursa ya viwanda hata vidogo kwani dhamira ni kuona waTanzania wengi zaidi wanamiliki viwanda. 
  • Kwa kuwa Rais wetu Mh Dr. John Pombe Joseph Magufuli amedhamiria kutumia vizuri fedha ya serikali kuwaletea wananchi maendeleo; awataka waunge mkono juhudi zake kwa kutoa risiti ili walipe kodi halali. 
  • Aeleza fursa za uwekezaji zilizopo na mipango ya Wilaya kukuza biashara na uchumi.
  • Awashauri kujiunga na TCCIA ili wapate sauti ya pamoja. na awataka kuchagua wajumbe wa baraza la biashara. 
  • Aahidi kufanya kikao cha baraza mwezi Mei, 2018.
Picha ya Pamoja Mara Baada ya Kikao






Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkt. TCCIA - W., Mkt. wa halmashauri na kaimu DED, Mkiti wa mamlaka ya mji mdogo na TEO. Pia wakuu wa idara za Halmashauri. Kilifanyika Tar. 27/03/2017 Katika ukumbi wa Kimweri.




Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Mwigulu Lameck Nchemba Awa Waziri wa kwanza kufika Kijiji cha Makasa, Kata ya Kirangare, Wilaya ya Same.
  • Apanda milima ambayo wengi wanaigopa.
  • Ahimiza Umuhimu wa amani na kila mtu kuhakikisha inalindwa.
  • Atangaza hatari kwa wastawishaji wa mirungi, kwani sheria mpya inaruhusu kutaifisha mashamba.
  • Ashiriki Harambee ya ujenzi wa kanisa. 
  • Wananchi waipongeza serikali ya awamu ya Tano, kwani hawajawahi kutembelewa na Waziri. 
  • Wananchi waomba asaidie kuiomba serikali watengenezewe barabara.
  • Naye Askofu Mjema wa KKKT Dayosisi ya Pare Apongeza kazi nzuri inayofanywa na serikali
Mkuu wa Wilaya Same Apongeza kazi kubwa iliyofanywa Wilayani ya kuondoa mirungi.


Mh. Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, akiwa katika Picha ya Pamoja Mara Baada ya Kumalizika kwa Ibada.
 
TAHOSA YAPANIA KUPANDISHA UFAULU SAME.

Kikao cha Wakuu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Same chafanyika Tar. 21/03/2018.

  • 🔰 Wakusudia kutoka nafasi 21 hadi ya kumi bora kitaifa..
  • 🔰Wajipongeza kuongeza ufaulu toka nafasi ya 68 hadi 21.
  • 🔰Waeleza changamoto ya utoro wa wanafunzi kama kikwazo cha ufaulu.
  • 🔰Wamuomba DC kuwa mlezi wao.
DC Same aliyekuwa mgeni rasmi kwenye kikao hizo afanya yafuatayo.
  • Atoa zawadi kwa shule 3 za kwanza kwa ujumla na 3 za serikali
  • Awapongeza waliofanya vizuri kwa kuungana na kauli ya Same ya kutaka mabadiliko.
  • DC aeleza baadhi ya sababu zinazopelekea shule za binafsi kufanya vizuri kuliko za serikali
" Tulijaribu kufanya uchambuzi mwaka jana na tulijifunza kuwa watoto wanaokaa nyumbanj(day) wengi wana wanamaadili mabaya kuliko wale wa bording/ hostel kwani wazazi hawafuatilii ratiba za watoto kama Mwl. anavyofuatilia shuleni. wanawaacha watoto waende wanakotaka bila kujali wanafanyanini na hii inapelekea watoto kujiingiza kwenye mambo yasiyohusiana na masomo; Wakati mtoto anayesoma bording muda wote ana ratiba inayojulikana na kufuatiliwa, hivyo kumpelekea mtoto kuzingatia masomo muda mwingi na kupelekea kufanya vizuri zaidi." Na kwa kuwa shule nyingi za binafsi ni za bording ndiyo inawapelekea kufanya vizuri zaidi.

  • Asema pia uzembe wa baadhi ya walimu ni changamoto. Atoa Mf. wa matokei ya 2016 ambapo baada ya hesabu somo lililofuata kwa matokeo mabaya ni history ambayo ina walimu hadi wa ziada; haina practical lakini bado wameshindwa kuwaelewesha watoto.
  • Atoa wito kwa walimu wazembe kukaza buti kudhihirisha uwezo wao kwa vitendo. Maana siku zao zinahesabika.
  • Awakumbusha kumtendea haki Rais wetu Mh. Dr. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na serikali na watanzania kwani ameboresha Elimu pamoja na kuwapa posho ya madaraka.
  • Awataka WEO/ VEO kuwaelimisha wazazi juu ya chakula cha mchana ili wakae muda mwingi mchana wakiwa na uangalizi wa shule.
  • Agawa kitabu cha maadili ya watoto wa kike kwa kila shule, na awaomba walimu kuendelea kuwaelimisha ili kuondokana na mimba.
  • Apongeza kwa takwimu zinazoashiria kupungua kwa mimba kulinganisha na 2017.
  • Awataka shule zilizofanya vibaya kujithathmini ili kuongeza ufaulu.
  • Awakumbusha shule binafsi kubadilishana uzoefu na wenzao ili kufanya vizuri kama taifa.
" Huko nyuma matokeo yalipokuwa mabaya, kila mtu alimtaja mwenzake kuwa ndiye aliyefanya uzembe( walimu walisema ni serikali na wazazi; wazazi walisema ni walimu na serikali; na serikali tumesema ni wazazi na walimu wazembe;
Lakini sasa tumefanya vizuri kila ninayekutana naye anaeleza jinsi alivyochangia /Alivyohusika na ufaulu huo, na kama ni hivyo basi kila mtu akubali pia alihusika kwa kufanya vibaya". Asema DC Same Mh. Rosemary Senyamule.

  • Awataka wadau wote kutimiza wajibu wao, ili tujivunie matokeo mazuri kwa pamoja.
  • Tanzania ya viwanda inahitaji wataalamu.
" Same is not same" 
Image may contain: 12 people, people smiling, people standing and shoes
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Same akiwa na Wajumbe wa YAHOSA mara baada ya Kikao.




NGO ya VOEWOF yadhamiria kuimarisha matumizi ya nishati mbadala Wilayani Same..
Katika kikao kilichofanyika Tar 20/03/2018. Wadau wa mazingira walieleza sababu zinazopelekea watu kutochangamkia nishati mbadala pamoja na juhudi za serikali na wadau kuhimiza matumizi yake.
Baadhi ya sababu zinazotajwa ni:-
  • Kutopatikana nishati hiyo vijiji Mf. gas
  • Gharama kubwa ya nishati mbadala, pia kodi katika bidhaa hizo.
  • Mazoea na utamaduni
Ambapo nishati ya kutumia Mkaa na kuni vinapelekea uharibifu mkubwa wa mazingira na upungufu wa maji.
  • 💡Wadau wakubaliana kuongeza matumizi, kubuni na kuanzisha nishati mbadala yenye gharama nafuu, 
  • 💡kuendelea kuelimisha juu ya athari ya mazingira na uwepo wa nishati mbadala.
  • 💡Kuhimiza matumizi ya "interlocking block" badala ya tofari za kuchoma.
  • 💡Kusimamia sheria.
  • 💡Shirika la VOEWOF linalofanya kazi chini ya CARE International linafanya kazi na vikundi vya wanawake. 
  • 💡limewezesha majiko ya gas zaidi ya 300 kutumika vijijini. 
  • 💡Limepania kuanzisha viwanda vya kutengeneza nishati mbadala kwa kutumia taka. 
  • 💡Wilaya yaahidi kutoa eneo, kutoa mikopo kwa vikundi hivyo na kutumia miti inayooteshwa na vikundi hivyo.

Kikao hicho pia kimewashirikisha DC wa Same, wataalamu toka ofisi ya RC Kilimanjaro na halmashauri ya Same, TBS, wanazuoni toka SUA, TRA, wauzaji wa nishati mbadala, wanavikundi hao na vyombo vya habari.
DC Same alipongeza na kuwashukuru VOEWOF Na wadau wengine jinsi wanavyoshiriki kuibadilisha Same, kila mmoja kwenye nyanja yake. Alikiri kuwa kwa kasi hii; Wilaya ya Same itafikia malengo yake ya kubadili mazingira ya Same.

      




" Same is not same"
Wilaya Ya Same Ina Jumla ya Kata 35

B

  • Bendera
  • Bombo
  • Bwambo

C

  • Chome

H

  • Hedaru

K

  • Kalemawe
  • Kihurio
  • Kirangare
  • Kisima 
  • Kisiwani

L

  • Lugulu 

M

  • Mabilioni
  • Makanya 
  • Maore
  • Mhezi
  • Mpinji
  • Mshewa
  • Msindo 
  • Mtii
  • Mwembe 
  • Myamba

N

  • Ndungu
  • Njoro 

R

  • Ruvu 

S

  • Same Mjini
  • Stesheni 
  • Suji
  • Saweni

T

  • Tae

V

  • Vudee
  • Vuje
  • Vumari
  • Vunta
Karibu Tena Same

Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo